Pages

Friday, June 25, 2021

Mbegu bora za Karanga zinazotoa mafuta mengi

 



Tunazo mbegu aina mbili za karanga:

MNANJE 2009
• Hukomaa kwa siku 110 – 120.
• Hutoa mavuno ya wastani wa tani 1.5 - 2 kwa hekta.
• Ina mafuta wastani wa asilia 51.
• Ina kiasi kikubwa cha madini chuma – 65.4 mg/kg
• Punje kubwa, tamu.

NALIENDELE 2009
• Hukomaa kwa siku 90 – 100.
• Hutoa mavuno ya wastani wa tani 1 - 1.5 kwa hekta.
• Inavumilia ukame
• Hustahimili ugonjwa wa ukoma (rosette).

Tupigie: 0755325442

Rieta Seed kuongeza uzalishaji wa mbegu bora za karanga nchini Tanzania

Rieta Seed kipeperushi cha mbegu bora za karanga
Kipeperushi cha mbegu bora za karanga zinazozalishwa na Rieta Seed kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti Tanzania (TARI) na wadau wengine.

Rieta Seed rollup banner
Sifa za mbegu bora za karanga zinazozalishwa na kampuni ya mbegu Rieta Seed

Mbegu bora za karanga.

Karanga ni moja kati ya mazao muhimu sana ya mafuta. Mbegu zake huwa na kiasi kikubwa cha mafuta (38% – 50%), protini, kalishamu, potashiamu, fosiforasi, magnesiamu na vitamini. Inasadikiwa kuwa karanga pia zina aina fulani ya viini vinavyotumika kama dawa. Zao hili linazalisha katika maeneo mengi nchini. 


UTANGULIZI

Karanga ni zao muhimu la mafuta, ambalo hutumika kama chakula cha binadamu. Mashudu na majani yake hutumika kulisha mifugo. Pia hurutubisha udongo. Tanzania ni nchi ya pili kwa uzalishaji wa karanga Afrika baada ya Naijeria.

 

MAZINGIRA YA UZALISHAJI

Hali ya hewa

  • Karanga hustawi vizuri katika maeneo yenye mwinuko chini ya mita 1,500 kutoka usawa wa bahari.
  • Huhitaji mvua ya wastani wa milimita 500 – 1,200 kwa mwaka.
  • Pia hustawi vizuri kwenye udongo wa kichanga wenye rutuba.

 

Utayarishaji wa shamba

  •      Tifua vizuri shamba ili kuwezesha udongo kupenyesha maji na mizizi kirahisi.
  •      Karanga hupandwa kwenye matuta au sesa.

 

Kuchagua mbegu za kupanda

Hakilisha unapata mbegu bora zilizo thibitishwa kitaalamu na kuainisha na Taasisi za utafiti wa Kilimo.

 

Aina za karanga

Kuna aina nyingi za karanga ambazo zimefanyiwa utafiti na kuidhinishwa zitumike kwa wakulima. Kati ya hizo, Rieta Seed inazalisha mbegu mbegu mbili ambazo ni;

 

MNANJE 2009

  • Hukomaa kwa siku 110 – 120.
  • Hutoa mavuno ya wastani wa tani 1.5 - 2 kwa hekta.
  • Ina mafuta wastani wa asilia 51.
  • Ina kiasi kikubwa cha madini chuma – 65.4 mg/kg
  • Punje kubwa, tamu.

 

NALIENDELE 2009

  • Hukomaa kwa siku 90 – 100.
  • Hutoa mavuno ya wastani wa tani 1 - 1.5 kwa hekta.
  • Inavumilia ukame
  • Hustahimili ugonjwa wa ukoma (rosette).

UPANDAJI

  • Mbegu zipandwe mapema wa mvua za kwanza.
  • Karanga zipandwe kwa nafasi ya sentimeta 10 kati yam mea na sentimeta 50 kati ya mistari.
  • Mahitaji ya mbegu kwa hekta ni kilo 80 hadi 100.
  • Ipandwe mbegu/punje moja kwenye shimo la kina kati ya sentimeta 2.5 hadi 5.

 

PALIZI

  • Palizi ya kwanza ifanyike majuma mawili baada ya karanga kuota.
  • Palizi ifanyike mara mbili hadi tatu kuzuia magugu.

KUDHIBITI WADUDU NA MAGONJWA

Magonjwa

1.        Ugonjwa wa Ukoma (Rosette Virus Disease)

  • Huenezwa na wadudu waitwao vidukali (Aphid)
  • Mimea iliyoshambuliwa hudumaa, majani kukunjamana na kuwa na rangi ya manjano.
  • Unaweza kuathiri mavuno hadi 100%.

 

2.        Ugonjwa wa madoa ya majani (Leaf spots)

  • Ugonjwa huu ni wa aina mbili yaani Madoa change (Early leaf spot) na Madoa pevu (Late leaf spot).
  • Unaweza kuathiri mavuno hadi 30%.

 

3.        Ugonjwa wa kutu ya majani (Rust)

  • Husababishwa na vimelea vya Puccinia arachidis
  • Jani huwa na vipele vya rangi ya kahawia hasa chini ya jani.

 

4.        Sumu kuvu ya karanga (Aflatoxin)

  •   Katika hali ya unyevu mwingi vimelea viitwavyo Aspegilus flavus huota ndani ya maganda na kushambulia mbegu za karanga.
  •   Vimelea hivyo hutoa kemikali ambayo ni sumu.

Kudhibiti magonjwa

Ni vema kuzingatia kanuni za kilimo bora hasa kwa kutumia mbegu bora zenye ukinzani, kupanda mapema, kupanda katika nafasi zilizopendekezwa, kupalilia kwa wakati, kuvuna kwa wakati, kukausha mavuno mara baada ya kuvuna na kuhifadhi mahali pasipo na unyevu.

 

Wadudu waharibifu

  • Karanga hushambuliwa hasa na Vidukari ambao hueneza ugonjwa wa Ukoma.
  • Inzi wa karanga, mchwa, panya na ndege.
  • Dhibiti kwa kupanda mapema, kupanda kwa nafasi, kutumia kilimo mseto, kuvuna na kuhifadhi kwa mfumo wa Mandela Kock na kupulizia viuatilifu inapolazimu.

 

UVUNAJI NA UHIFADHI

Vuna baada ya kukomaa kwa jembe la mkono au kung’oa.

Kausha vizuri kwenye jua kwa muda wa wiki 2-3 hadi kufikia unyevu wa chini ya 13%.

Karanga zilizokauka vizuri hutoa mlio ukitikisa ganda lake.

Hifadhi kwenye ghala kavu zikiwa kwenye magunia yanayopitisha hewa na zikiwa na maganda yake.

Ubora na uwezo wa karanga kuota huanza kupotea baada ya kubanguliwa.

Friday, June 4, 2021

Rieta yajipanga kukabiliana na upungufu wa mbegu za karanga nchini

 

Mtaalamu wa kilimo ndugu Eliud Musumi akikagua shamba darasa la Rieta Seed na kutoa maelekezo ya namna bora ya kuvuna zao la karanga. 

Kutokana na tatizo la upungufu wa mafuta nchini, wakulima wanapaswa kuongwza uzalishaji wa mazao ya mafuta zikiwemo karanga. Ili kupata mavuno mengi na bora ya karanga wakulima wanatakiwa kuzingatia matumizi ya mbegu bora za karanga zenye mavuno mengi, zinazotoa mafuta kwa wingi na zinazokabiliana na magonjwa mbalimbali shambani.

Kwa kukabiliana na matatizo hayo, kampuni ya mbegu ya RIETA inazalisha mbegu bora za karanga zenye mavuno mengi, zinazotoa mafuta kwa wingi na zinazokabiliana na magonjwa mbalimbali shambani. 

Tunawasihi wakulima wote kutumia mbegu bora za karanga ili waongeze uzalishaji wa zao hili tupunguze tatizo la uhaba wa mafuta ya kula nchini. 

Rieta AgroSciences Tanzania Limited ni Kampuni ya kizalendo inayojishughulisha na usambazaji wa pembejeo za kilimo kwa wakulima. 

Dhamira ya Rieta ni kuwafanya wakulima waweze kutatua changamoto zinazowakabili kibunifu zaidi. Dhamira hii itawezekana kupitia utafiti, uzalishaji, uchakataji na usambazaji wa mbegu bora za mazao mbalimbali zenye kustahimili changamoto za kimazingira ikiwemo ukame, magonjwa na wadudu mbalimbali. 

Mbegu zingine zinazozalishwa na RIETA ni mahindi (UH 6303 na Situka M1), Mtama (Macia) na alizeti (Record).


Mbegu bora za karanga