Kipeperushi cha mbegu bora za karanga zinazozalishwa na Rieta Seed kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti Tanzania (TARI) na wadau wengine. |
Sifa za mbegu bora za karanga zinazozalishwa na kampuni ya mbegu Rieta Seed |
Mbegu bora za karanga. |
Karanga ni moja kati ya mazao muhimu sana ya mafuta. Mbegu zake huwa na kiasi kikubwa cha mafuta (38% – 50%), protini, kalishamu, potashiamu, fosiforasi, magnesiamu na vitamini. Inasadikiwa kuwa karanga pia zina aina fulani ya viini vinavyotumika kama dawa. Zao hili linazalisha katika maeneo mengi nchini.
UTANGULIZI
Karanga
ni zao muhimu la mafuta, ambalo hutumika kama chakula cha binadamu. Mashudu na
majani yake hutumika kulisha mifugo. Pia hurutubisha udongo. Tanzania ni nchi
ya pili kwa uzalishaji wa karanga Afrika baada ya Naijeria.
MAZINGIRA YA
UZALISHAJI
Hali ya hewa
- Karanga hustawi vizuri katika maeneo yenye mwinuko chini ya mita 1,500 kutoka usawa wa bahari.
- Huhitaji mvua ya wastani wa milimita 500 – 1,200 kwa mwaka.
- Pia hustawi vizuri kwenye udongo wa kichanga wenye rutuba.
Utayarishaji wa shamba
- Tifua vizuri shamba ili kuwezesha udongo kupenyesha maji na mizizi kirahisi.
- Karanga hupandwa kwenye matuta au sesa.
Kuchagua mbegu za kupanda
Hakilisha
unapata mbegu bora zilizo thibitishwa kitaalamu na kuainisha na Taasisi za
utafiti wa Kilimo.
Aina za karanga
Kuna
aina nyingi za karanga ambazo zimefanyiwa utafiti na kuidhinishwa zitumike kwa
wakulima. Kati ya hizo, Rieta Seed inazalisha mbegu mbegu mbili ambazo ni;
MNANJE 2009
- Hukomaa kwa siku 110 – 120.
- Hutoa mavuno ya wastani wa tani 1.5 - 2 kwa hekta.
- Ina mafuta wastani wa asilia 51.
- Ina kiasi kikubwa cha madini chuma – 65.4 mg/kg
- Punje kubwa, tamu.
NALIENDELE 2009
- Hukomaa kwa siku 90 – 100.
- Hutoa mavuno ya wastani wa tani 1 - 1.5 kwa hekta.
- Inavumilia ukame
- Hustahimili ugonjwa wa ukoma (rosette).
UPANDAJI
- Mbegu zipandwe mapema wa mvua za kwanza.
- Karanga zipandwe kwa nafasi ya sentimeta 10 kati yam mea na sentimeta 50 kati ya mistari.
- Mahitaji ya mbegu kwa hekta ni kilo 80 hadi 100.
- Ipandwe mbegu/punje moja kwenye shimo la kina kati ya sentimeta 2.5 hadi 5.
PALIZI
- Palizi ya kwanza ifanyike majuma mawili baada ya karanga kuota.
- Palizi ifanyike mara mbili hadi tatu kuzuia magugu.
KUDHIBITI WADUDU NA MAGONJWA
Magonjwa
1.
Ugonjwa wa Ukoma (Rosette Virus Disease)
- Huenezwa na wadudu waitwao vidukali (Aphid)
- Mimea iliyoshambuliwa hudumaa, majani kukunjamana na kuwa na rangi ya manjano.
- Unaweza kuathiri mavuno hadi 100%.
2.
Ugonjwa wa madoa ya majani (Leaf spots)
- Ugonjwa huu ni wa aina mbili yaani Madoa change (Early leaf spot) na Madoa pevu (Late leaf spot).
- Unaweza kuathiri mavuno hadi 30%.
3.
Ugonjwa wa kutu ya majani (Rust)
- Husababishwa na vimelea vya Puccinia arachidis
- Jani huwa na vipele vya rangi ya kahawia hasa chini ya jani.
4.
Sumu kuvu ya karanga (Aflatoxin)
- Katika hali ya unyevu mwingi vimelea viitwavyo Aspegilus flavus huota ndani ya maganda na kushambulia mbegu za karanga.
- Vimelea hivyo hutoa kemikali ambayo ni sumu.
Kudhibiti
magonjwa
Ni vema kuzingatia kanuni za kilimo bora
hasa kwa kutumia mbegu bora zenye ukinzani, kupanda mapema, kupanda katika
nafasi zilizopendekezwa, kupalilia kwa wakati, kuvuna kwa wakati, kukausha
mavuno mara baada ya kuvuna na kuhifadhi mahali pasipo na unyevu.
Wadudu
waharibifu
- Karanga hushambuliwa hasa na Vidukari ambao hueneza ugonjwa wa Ukoma.
- Inzi wa karanga, mchwa, panya na ndege.
- Dhibiti kwa kupanda mapema, kupanda kwa nafasi, kutumia kilimo mseto, kuvuna na kuhifadhi kwa mfumo wa Mandela Kock na kupulizia viuatilifu inapolazimu.
UVUNAJI NA UHIFADHI
Vuna baada ya kukomaa kwa jembe la mkono au kung’oa.
Kausha vizuri kwenye jua kwa muda wa wiki 2-3 hadi kufikia unyevu wa chini ya 13%.
Karanga zilizokauka vizuri hutoa mlio ukitikisa ganda lake.
Hifadhi kwenye ghala kavu zikiwa kwenye magunia yanayopitisha hewa na zikiwa na maganda yake.
Ubora na uwezo wa karanga kuota huanza kupotea baada ya kubanguliwa.
No comments:
Post a Comment